• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Acacia yafutwa katika soko la hisa

    (GMT+08:00) 2019-11-18 19:16:12
    Baada ya miaka minane ya kudumu katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), kampuni ya Acacia imefutwa rasmi kwenye soko hilo. Kampuni hiyo, iliyoorodheshwa DSE Desemba 2011 ikijulikana kama African Barrick Gold (ABG) kabla haijabadili jina na kuitwa Acacia Novemba 2014, inaondolewa sokoni hapo baada ya kukamilisha utaratibu wa kufutwa.

    Kufutwa kwa kampuni hiyo, taarifa zinaonyesha kutapunguza ukubwa wa mtaji wa soko hilo kutoka Sh19.67 trilioni uliokuwapo mwishoni mwa wiki iliyopita hadi Sh16.94 trilioni.

    Wakati ukubwa wa mtaji wa soko zima ukipungua, ule wa kampuni za ndani, Sh9.01 trilioni, hautabadilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako