• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Isuzu yamtuza Eliud Kipchoge gari jipya lenye thamani ya Sh4.1 milioni

    (GMT+08:00) 2019-11-18 19:16:33

    Kampuni ya ISUZU East Africa hatimaye imemtuza bingwa wa marathon mbio za Olympic Eliud Kipchoge, gari jipya aina ya Isuzu Single Cabin lenye thamani ya kiasi cha Sh4.1 milioni Jumamosi baada ya ufanisi mkubwa wa kuwa binadamu wa kwanza kukimbia mbio za marathon kwa muda chini ya saa mbili za 'Ineos 159 Challenge' Oktoba 2019.

    Mwenyekiti wa kampuni ya Isuzu World ambayo ni maarufu kwa uundaji, utengenezaji na ukarabaiti wa magari Eisaku Akazawa amekuwa nchini akitokea Japan ili kumtuza Kipchoge katika hafla iliyoandaliwa katika Msitu wa Karura.

    Hii ilikuwa ni baada ya mwanariadha huyo aliyekuwa na mkewe Grace pamoja na watoto wao watatu, kuongoza washiriki wapatao 200 wakiwemo wanafunzi, kukimbia umbali wa kilomita nne hapo Karura.

    Oktoba 12, 2019, Kipchoge alitumia muda wa 1:59:41 kukamilisha mbio za "Ineos 1:59 Challenge" jijini Vienna, Austria.

    Gari alilotuzwa lina nambari za usajili KCW 159V, ambapo "159V" inaendana na muda wa saa 1:59 na V kuwakilisha jiji la Vienna.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako