• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi wa Hong Kong wawataka watu wanaofanya vurugu na kujificha katika Chuo Kikuu cha Polytechnic kujisalimisha

    (GMT+08:00) 2019-11-18 19:35:55

    Polisi wa Hong Kong wamewataka watu wanaofanya vurugu waliojificha katika Chuo Kikuu cha Polytechnic mjini humo kuacha vitendo vya kimabavu na kujisalimisha.

    Kamanda wa eneo la Kowloon Magharibi Cheuk Hau-yip leo amesema, baada ya watu hao kukalia Chuo Kikuu hicho tarehe 11, wamefanya uharibifu mkubwa, wakichoma moto na kutengeneza mabomu ya gesi ndani ya chuo hicho, na hata kuwashambulia wakazi waliobomoa vizuizi walivyoweka katika sehemu ya karibu na kusababisha polisi mmoja kujeruhiwa mguuni.

    Msimamizi mkuu wa polisi wa mahusiano na umma Kwok Ka-chuen amesema, katika wiki moja iliyopita, watu hao wamefunga barabara, kuwarushia mabomu watumiaji wa barabara na kutishia maisha ya watu milioni 7 wa Hong Kong, kwa madai ya kutimiza "dhamira ya kisiasa", na kusema vitendo vyao ni vya ubinafsi na uovu. Vyuo vikuu vitatu vya Chinese, Polytechnic na City vimetoa ripoti kwa polisi vikisema watu hao wameficha mabomu mengi ya gesi vyuoni, na kuiba kemikali nyingi za kulipuka.

    Tangu mwezi Juni, watu 4,491 wamekamatwa na polisi kwa kuhusika na vurugu hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako