• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mafuriko yaathiri zaidi ya watu laki 5 nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2019-11-18 19:52:03

    Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema, mafuriko katika sehemu mbalimbali nchini Somalia yamewaathiri watu zaidi ya laki 5, huku watu 370,000 wakiondolewa katika makazi yao na pia kusababisha uharibifu wa miundombinu nchini humo.

    Ikinukuu takwimu kutoka Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) ofisi hiyo imesema watu karibu 17 wamefariki tangu mafuriko hayo yatokee tarehe 21 mwezi uliopita. Mashirika ya kibinadamu ya Umoja huo na wadau wake yamefanikiwa kuwafikia watu 105,000 walioathiriwa na mafuriko hayo, lakini bado msaada wa mahitaji ya muhimu unatakiwa.

    Ofisi hiyo imesema, wilaya zilizoathiriwa zaidi ni Beletweyne mkoani Hirshabelle ambapo watu 231,000 wamekimbia makazi yao na Bardheere mkoani Gedo, ambapo watu elfu 55 wameondoka kwenye makazi yao kutokana na mafuriko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako