• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Walinzi wa amani wa China waenda nchini Sudan Kusini kwa kipindi cha mwaka mmoja

    (GMT+08:00) 2019-11-19 16:06:29

    Jumla ya askari 240 wa kulinda amani kutoka China wameelekea Sudan Kusini wakitokea mji wa Zhangjiakou, mkoani Hebei kaskazini mwa China, kutekeleza majukumu ya ulinzi wa amani kwa kipindi cha mwaka mmoja.

    Askari hao wanajumisha kikosi cha kwanza cha askari 700 wa kulinda amani kutoka China, na watakuwa na majukumu ya ulinzi, kufanya doria, kusindikiza, kusuluhisha migogoro, kurejesha utulivu, kuokoa na majukumu mengine ya kiusalama.

    Kamanda wa kikosi hicho, Han Tao, amesema askari wote wamepitia mafunzo ya miezi mitatu yaliyoandaliwa kwa kufuata hali ya usalama nchini Sudan Kusini na kufaulu mafunzo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako