• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kundi la Taliban lawaachia huru raia wa Marekani na Australia waliowateka nyara

  (GMT+08:00) 2019-11-19 19:22:37

  Kundi la Taliban leo limewaachia huru wateka wawili raia wa Marekani na Australia ikiwa ni sehemu ya kubadilishana wafungwa, ambapo viongozi wa ngazi ya juu wa kundi hilo pia waliachiwa huru.

  Kituo cha Televisheni cha ITVNews kimesema, kundi hilo limewaachia huru Kevin King na Timothy Weeks, wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Marekani nchini Afghanistan.

  Mapema leo, vyombo vya habari nchini Afghanistan viliripoti kuwa, serikali ya nchi hiyo imewaachia huru wafungwa muhimu watatu wa kundi la Taliban, akiwemo Annas Haqqani, ili kufanikisha kuachiwa huru kwa wahadhiri hao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako