• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uganda yaomba upya mkopo wa SGR

    (GMT+08:00) 2019-11-19 19:32:41
    Uganda imetuma upya maombi ya mkopo wa kujenga reli ya kisasa ya kilomita 271 kati ya mji mkuu Kampala na mpaka wake na Kenya.

    Mratibu wa ujenzi wa reli hiyo Perez Wamburu amesema maombi hayo yametumwa kwa Benki ya Exim ya China na Uganda inatarajia mkopo wa asilimia 85 ya ufadhili wa mradi huo.

    Gharama ya mradi huo pia imepunguzwa kwa dola milioni 26.

    Mkopo wa awali ulichelewa kutokana na kuchelewa kwa upembuzi yakinifu,lakini sasa tayari umewasilishwa.

    Uganda tayari imetambua kilomita 126 za ukanda wa SGR kati ya Malaba-Kampala na upatikanaji wa ardhi unatarajiwa kuhitimishwa Juni 2022.

    Reli ya Uganda baadaye itaunganisha nchi jirani za Kenya, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako