• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanawake, vijana wafaidi Programu ya IIdea

  (GMT+08:00) 2019-11-19 19:33:49
  Wanawake na vijana 25,000 kutoka katika Nchi sita za Jumuiya ya Africa Mashariki (EAC) wamefaidika na miradi mbalimbali ya ujasiriamali kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Ujerumani (Giz) kupitia programu ya IIdea.

  Kaimu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Africa Mashariki Christophe Bazivumo akiongea na waandishi wa Habari mara baada ya kuzindua kikao cha siku nne, cha wadau wa Nchi wanachama wa EAC.Picha na Daniel Sabuni, Arusha

  Joiyce Kimaro, Mshauri Mkuu wa Programu ya IIdea, amesema wananchi hao wamewezeshwa kwa kubuni wazo la biashara ambalo linahusisha au kugusa sekta mbili zilizomo ndani ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Amesema mawazo hayo yalipitishwa kwenye programu hiyo iliyoanza kutekelezwa Mwaka 2016 na kupatiwa elimu ya biashara husuani masoko na jinsi kufanya biashara na kupata faida.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako