• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Taifa Stars yashindwa kuonesha makali yake dhidi ya Libya mechi ya kufuzu Afcon

    (GMT+08:00) 2019-11-20 08:21:27

    Tanzania imeshindwa kulinda bao la mapema baada ya kuwaruhusu Libya kutoka nyuma kipindi cha pili na kushinda 2-1 katika mchezo wa Kundi J kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2021 usiku wa jana Uwanja wa Mustapha Ben Jannet mjini Monastir, Tunisia.

    Pamoja na kufungwa, Tanzania inaendelea kushika nafasi ya pili katika Kundi J ikiizidi kwa wastani wa mabao tu Libya baada ya wote kufungana kwa pointi, tatu kila timu. Goli la Taifa Stars liliingizwa kimiani na nahodha Mbwana Ally Samatta katika dakika ya 18 kwa kupiga mkwaju wa penalti baada ya winga Simon Happugod Msuva kuangushwa na Mohamed Aleyat kwenye boksi. Katika mechi nyingine ya kundi hilo jana, Equatorial Guinea ilifungwa nyumbano 1-0 na Tunisia Uwanja wa Nuevo mjini Malabo. Taifa Stars itarejea Tunisia Agosti 31 mwakani kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza katika kundi hilo dhidi ya wenyeji, siku ambayo Libya watakuwa wenyeji wa Equatorial Guinea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako