• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Harambee Starlets yafanya maangamizi yaibanjua Djibout kwa mabao 12-0

    (GMT+08:00) 2019-11-20 08:22:08

    Timu ya soka ya Taifa ya Wanawake ya Kenya Harambee Starlets jana iliinyeshea Djibout mvua ya magoli 12-0, huku wachezaji wao watatu wakifunga hat-trick katika mashindano ya Kombe la Chalenji Cecafa kwa wanawake kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Matokeo hayo yanaifanya Kenya kufikisha pointi sita sasa ikisubiri mshindi wa mchezo wa pili wa Uganda dhidi ya Ethiopia ili kujua kama imefuzu nusu fainali au la. Kipigo hicho kwa Djibouti inayoshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza ni cha pili baada ya kufungwa na Uganda mabao 13 katika mchezo wa awali. Kwenye mechi ya kwanza ya mashindano hayo, Kenya ilianza vyema mechi za Kundi B kwa kuichapa Ethiopia 2-0. Katika kundi hilo pia kuna Uganda, ambao Starlets watachuana nao Alhamisi, Novemba 21.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako