• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Canada yaishinda Marekani na kuingia robo fainali ya Davis Cup

    (GMT+08:00) 2019-11-20 08:22:28

    Canada limekuwa taifa la kwanza kufikia robo fainali kwenye michuano ya Davis Cup baada ya kuinyuka Marekani kwa mara ya kwanza katika kampeni zao za mara 16. Vasek Pospisil alimshinda Reilly Opelka na Denis Shapovalov alimbanjua Taylor Fritz ambapo wawili hao wameendeleza ushindi wao walioupata katika mchuano wa kwanza dhidi ya Italia. Kichapo hicho ni cha kwanza kwa majirani hao wa Amerika kaskazini tangu mwaka 1965. Awali Wafaransa Nicolas Mahut na Pierre-Hugues Herbert walitoka nyuma na kushinda kwa 2-1 kwenye kundi A dhidi ya mahasimu wao Japan. Mabingwa hao wa Australian Open waliwatoa makamasi Ben McLachlan na Yasutaka Uchiyama 6-7 (4-7) 6-4 7-5 katika seti ya tatu. Na kwa upande wa Jo-Wilfried Tsonga alimwangamiza Uchiyama kwa 6-2 6-1 kwenye mechi ya mchezaji mmoja mmoja kabla ya mchezaji namba kumi duniani Gael Monfils kushindwa kwa 7-5 6-2 na Yoshihito Nishioka. Ufaransa itavaana na Serbia kesho Alhamis.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako