• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAO yasema Sudan Kusini yakabiliwa na ukosefu wa tani laki 7 za chakula

    (GMT+08:00) 2019-11-20 08:39:44

    Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema, Sudan Kusini inakabiliwa na ukosefu wa tani laki 7 za chakula kutokana na athari za mafuriko.

    Mjumbe wa FAO nchini humo Bw. Meshack Malo, amesema mafuriko yameharibu maeneo mengi nchini humo katika majira ya mavuno, na kusababisha watu waliopoteza makazi na wakimbizi wapatao laki 9.08 kuathiriwa vibaya.

    Bw. Malo pia amesema licha ya kuongeza uwekezaji katika sekta ya kilimo ili kupunguza ukosefu wa chakula, msaada zaidi wa chakula pia unahitajika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako