• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mancini awatisha wapinzani Euro 2020

    (GMT+08:00) 2019-11-20 18:17:23
    Baada ya timu ya taifa ya Italia kufanikiwa kufuzu michuano ya Kombe la Euro 2020, kocha wa timu hiyo Roberto Mancini, amedai ubora wa kikosi chake utawafanya wapinzani wasiingize timu uwanjani. Timu hiyo ilikuwa kundi J, hivyo juzi ilifanikiwa kufuzu baada ya kuwachapa wapinzani wao Armenia mabao 9-1, huko jijini Palermo nchini Italia. Katika mchezo huo, Italia walionekana kuwa kwenye kiwango cha hali ya juu na kuwafanya mashabiki waamini kuwa timu hiyo ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kwenye michuano hiyo. Kichapo hicho kimemfanya kocha wa timu hiyo Mancini aamini hiyo ni salamu kwa wapinzani ambao watakuwa kundi moja na ikiwezekana wasipeleke timu uwanjani.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako