• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Wakenya wawili nje miaka minne kwa kutumia pufya

    (GMT+08:00) 2019-11-20 18:34:52

    Kitengo cha Maadili (AIU) katika Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF), kimemwondolea marufuku Mkenya John Kibet Kendagor, ambaye alikuwa ametuhumiwa kwa kutumia dawa za kusisimua misuli. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na AIU, Kendagor hakupatikana na hatia yoyote baada ya sampuli za damu yake kufanyiwa uchunguzi. Mwanariadha huyo alishiriki mbio za marathon za Istanbul nchini Uturuki, na Seoul nchini Korea Kusini mwaka 2017, alipopewa adhabu ya kutoshiriki mashindano yoyote yaliyofuata baada ya kukataa kutoa sampuli za damu kwa uchunguzi wa kiafya. Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Wakenya wengine Abraham Kiptum na Cyrus Rutto, kupewa adhabu ya kutoshiriki mbio zozote kwa miaka minne kila mmoja, kwa hatia ya kutumia pufya. Kendagor ni bingwa wa dunia mbio za Half Marathon.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako