• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapinga Baraza la juu la bunge la Marekani kupitisha "Sheria ya haki za binadamu na demokrasia kuhusu Hong Kong ya mwaka 2019"

  (GMT+08:00) 2019-11-20 18:36:56

  Kamati ya mambo ya nje ya Bunge la Umma la China leo imetoa taarifa likilaani vikali hatua ya Baraza la juu la bunge la Marekani kupitisha "Sheria ya haki za binadamu na demokrasia kuhusu Hong Kong ya mwaka 2019".

  Taarifa hiyo imesema Baraza hilo limepitisha sheria hiyo inayohusiana na Hong Kong bila kujali malalamiko na pingamizi la China, kitendo ambacho ni kuingilia mambo ya ndani ya China.

  Taarifa hiyo imesema, vitendo vya kimabavu vilivyotokea mkoani Hong Kong katika miezi mitano iliyopita vinahusiana na Marekani kuingilia kati mambo ya Hong Kong na mambo ya ndani ya China. Kuzuia vurugu na kurejesha hali ya utulivu wa Hong Kong ni kazi muhimu zaidi kwa sasa. Hata hivyo, Baraza la juu la bunge la Marekani linawaunga mkono wanaofanya vurugu mkoani Hong Kong kwa kisingizio cha "haki za binadamu" na "demokrasia", kitendo kinacho kimeonyesha vigezo viwili na nia mbaya ya Marekani dhidi ya China.

  Nayo Kamati ya mambo ya nje ya Baraza la mashauriano ya kisiasa la China leo imetoa taarifa kupinga sheria hiyo ya Marekani na kusema, kitendo chochote cha kuharibu ustawi na utulivu wa Hong Kong na kuzuia maendeleo ya China hakitafanikiwa kamwe.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako