• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuwabana wanaokwepa ushuru

    (GMT+08:00) 2019-11-20 18:40:20

    Serikali ya Kenya kupitia mamlaka yake ya Kodi KRA imesema inalenga kutumia mfumo wa kieletroniki ili kuhakikisha wafanya biashara wanaokwepa kulipa kodi wanashtakiwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Mkuu wa KRA Bw James Mburu amesema kuwa wazalishaji wote wenye vibali, waingizaji bidhaa, wasambazaji bidhaa, wauzaji wa rejareja na umma wote, wanatakiwa kuwa na nembo maalum ya ushuru.

    Naye kamishna wa Kodi za ndani KRA Bi Elizabeth Meyo amesema hivi sasa Kenya ina wazalishaji zaidi ya 130 na waingizaji wa maji ya chupa, juisi, soda, vinywaji vya kuongeza nguvu (Energy drinks) na vinywaji vingine visivyo na vileo ambao wameshasajiliwa katika mfumo wa kielektroniki wa Utambuzi wa Bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako