• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CIPLA yatuma shehena ya kwanza ya dawa Rwanda

    (GMT+08:00) 2019-11-20 18:41:04

    Kampuni ya kutengeneza madawa nchini Uganda Cipla imetuma shehena yake ya kwanza nchini Rwanda ikiwa ni sehemu kampeini ya rais ya Kumaliza ugonjwa wa Malaria PMI. Kampuni hiyo ilipatiwa kandarasi na PMI miezi kadhaa iliyopita kutengeneza na kusambaza dawa za kutibu ugonjwa wa Malaria Artemether Lumefrantrine kwa nchi za Afrika na zile zilizopo nje ya Afrika kama vile Myanmar ambazo hupokea dawa kupitia ufadhili wa PMI.Katibu mkuu mtendaji wa Cipla Nevin Bradford amesema wanafuraha kubwa kupatiwa jukumu la kutengeneza na kusambaza dawa za kutibu ugonjwa wa Malaria kwa gharama ya chini kwa wagonjwa kutoka Afrika na sehemu nyingine duniani. Amesema kampuni hiyo inalenga kuleta mabadiliko kwa wagonjwa na kuokoa maisha.PMI ilizinduliwa rasmi mwaka wa 2005 kwa ajili ya kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Malaria kwa asilimia 50 Nchi ya Rwanda ni mojawapo ya nchi ambazo zinakumbwa na tishio la ugonjwa wa Malaria hata hivyo imejitahidi kupiga hatua kubwa zaidi katika vita dhidi ya Malaria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako