• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachimba madini watakiwa kulipa ushuru wa huduma kwa jamii

    (GMT+08:00) 2019-11-20 18:41:42
    Waziri wa Madini nchini Tanzania Bw Dotto Biteko, amewataka wamiliki wa leseni za uchimbaji wa madini nchini pamoja na kampuni inayozalisha madini kulipa ushuru wa huduma ya uwajibikaji kwa jamii na kodi ya huduma.

    Biteko alitoa kauli hiyo mkoani Geita wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi kwenye zahanati ya gereza la Wilaya ya Geita inayojengwa kwa ufadhili wa Halmashauri ya Mji wa Geita na Mgodi wa GGML kupitia fedha ya wajibikaji wa makampuni. Pia waziri huyo amewataka wawekezaji nchini humo wa sekta ya madini kuzingatia sheria ya kuwapa kipaumbele wazawa katika ajira ,pamoja na biashara.

    Awali Mkuu wa gereza la Geita, Mussa Mkisi, alisema kuwa ujenzi wa zahanati hiyo ulianza mwezi julai mwaka huu ambapo sh. milioni 108 zimetumika kwa hatua ya kwanza.

    Biteko amesema kila mgodi unaomilikiwa na kikundi ,kampuni ambao unazalisha madini unatakiwa kulipa huduma ya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii na kodi ya huduma.

    Waziri huyo alisema wamiliki wa leseni za uchimbaji wa madini wanatakiwa kutambua kuwa tozo hizo si kwa kampuni kubwa pekee kama GGML bali ni kwa mgodi yote yenye leseni za uchimbaji zinazozalisha madini hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako