• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Huawei yaboresha mfumo wa huduma

    (GMT+08:00) 2019-11-20 18:48:20

    Kampuni ya simu ya China Huawei Cloud imeboresha mfumo wake wa huduma kwa kuanzisha mfumo uitwao Kunpeng ECS (Elastic Cloud Server).

    Mfumo huo unatajwa kuwa utaongeza ufanisi wa huduma, unafuu na uharaka.

    Mfumo huo wa kompyuta unatarajiwa kuanza kupatikana katika soko la Afrika mwishoni mwa Desemba mwaka huu.

    Hatua hiyo huenda ikawa neema kwa taasisi za umma na binafsi zinazotumia mifumo ya Tehama katika shughuli zake.

    Rais wa Huawei Ruis Houwei amesema wanakusudia kutoa huduma za kompyuta na wakati huo huo kufanya ubunifu wa hali ya juu ili kusaidia taasisi za umma, sekta binafsi na kampuni mbalimbali kuweza kutimiza malengo yao ya kukua zaidi.

    Houwei amesema mfumo huo mpya utakuwa na kasi zaidi kwa asilimia 15 na ufanisi wake ni asilimia 30 zaidi ukilinganishwa na mifumo mingine iliyopo sokoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako