• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Russia kuimarisha uungaji mkono kwa upande mwingine na kuanzisha ushirikiano wa kupinga uingiliaji

    (GMT+08:00) 2019-11-20 19:46:17

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China na Russia zina maslahi na mahitaji ya pamoja katika ulinzi wa mamlaka na usalama wa taifa, ulinzi wa utulivu na utaratibu wa jamii na kupinga uingiliaji kutoka nje.

    Amesema kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili, pande hizo zitaendelea kuimarisha uhusiano wa kiwenzi na kimkakati katika zama mpya kati ya nchi hizo, na kuzidi kufanya mawasiliano na kuungana mikono na kuanzisha ushirikiano wa kupinga uingiliaji wa nje, ili kulinda maslahi ya pamoja na amani na utulivu wa kikanda na dunia.

    Habari zinasema, wabunge wa Russia na wajumbe wa bunge la umma la China watakutana hapa Beijing na kujadiliana kuhusu kuzuia nguvu ya nje kuingilia kati siasa ya ndani na mamlaka ya taifa.

    Bw. Geng amesema, nchi hizo mbili zina imani na uwezo wa kupinga kithabiti uingiliaji wowote kutoka nje na kulinda ustawi na utulivu wa ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako