• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Jose Mourinho afika uwanja wa mazoezi wa Tottenham kuwaangalia vijana wake wapya

    (GMT+08:00) 2019-11-21 09:24:39

    Jose Mourinho jana alikwenda kwenye uwanja wa mazoezi wa Tottenham kukutana na kikosi chake kipya baada ya kutangazwa kuwa kocha mpya anayechukua nafasi ya Mauricio Pochettino kwenye klabu hiyo iliyokuwa ikijikokota katika ligi ya Premier. Meneja huyo wa zamani wa Chelsea, Real Madrid na Manchester United amekuwa kocha mpya baada ya Muargentina huyo kutimuiwa kazini. Mourinho mwenye miaka 56 ambaye hakuwa na kibarua chochote tangu alipoondoka United Disemba mwaka jana, amesaini mkataba hadi mwishoni mwa msimu wa 2022-23 . Klabu imefikia fainali ya Champions League mwezi Juni lakini ipo nafasi ya 14 kwenye Premier League baada ya kushinda gemu tatu tu kati ya 12. Wana pointi 11 nyuma ya timu nne za juu. Mourinho anajiunga na Tottenham akiwa na kumbukumbu ya kushinda mataji matatu ya EPL akiwa na Chelsea, huku akiwa na rekodi ya kuwa miongoni mwa makocha watatu pekee waliowahi kutwaa UEFA Champions League wakiwa na club mbili tofauti (FC Porto 2004, Inter Milan 2010).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako