• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kilimanjaro Queens yaingia nusu fainali kibabe CECAFA Challenge Wanawake

    (GMT+08:00) 2019-11-21 09:25:05

    Tanzania Bara imekamilisha mechi zake za Kundi A michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Wanawake kwa ushindi wa 7-0 dhidi ya Zanzibar jioni ya jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Matokeo hayo yanamaanisha Kilimanjaro Queens inamaliza kama kinara wa Kundi A kwa pointi zake tisa na mabao 20 ya kufunga, ikiwa haijafungwa hata bao moja hivyo kwenda Nusu Fainali kibabe na itakutana na mshindi wa pili wa Kundi B. Zanzibar inamalizia mkiani katika kundi hilo baada ya kufungwa mechi zote, nyingine 5-0 kila mechi dhidi ya Burundi na Sudan Kusini. Queens, mabingwa mara mbili mfululizo wa michuano hiyo, waliipiga 9-0 Sudan Kusini na 5-0 Burundi katika mechi zake mbili za mwanzo.

    Mechi za mwisho za Kundi B zitafanyika leo, Djibouti ikimenyana na Ethiopia kuanzia Saa 8:00 mchana na Kenya dhidi ya Uganda kuanzia Saa 10:30 jioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako