• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OLIMPIKI: Majaji na waamuzi wa masumbwi wa Olimpiki ya Rio marufuku kwenye Olimpiki ya Tokyo

    (GMT+08:00) 2019-11-21 09:25:23

    Kikosi kazi cha Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki kimesema hakuna mwamuzi au jaji hata mmoja kati 36 walioshiriki kwenye mashindano ya ndondi ya Olimpiki ya Rio 2016 ambao wanaruhusiwa kushiriki Olimpiki ya Tokyo 2020. Majaji na waamuzi kadhaa wamerejeshwa nyumbani kutoka Rio baada ya kufanya maamuzi mengi yanayotia shaka wakati wa mashindano ya masumbwi. Kwenye Olimpiki ya Tokyo, waamuzi na majaji watachaguliwa kutoka kwenye Shirikisho la Ndondi la Kimataifa AIBA ambao wanatambuliwa rasmi, na ambao wametathminiwa ili kuhakikisha wanafikia vigezo. Uchunguzi uliofanywa na AIBA mwaka 2017 haukugundua kosa lolote la kuingilia matokeo na kupendekeza kuwa majaji wa Rio wajumuishwe kulingana na kesi zao lakini vigezo vipya vya IOC vimefanya kuonekana hawafai kwa michezo ya Tokyo. Kikosi kazi kimesema uamuzi wao umekuja baada ya kuongea na wanamichezo ili kuongeza uwazi na uadilifu katika mchakato wa kuchagua majaji na waamuzi watakaoshiriki Olimpiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako