• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • VOLIBOLI: Michuano ya kabla ya msimu wa voliboli kutimua vumbi Disemba 7-8

    (GMT+08:00) 2019-11-21 09:25:40

    Michuano ya pili ya kabla ya msimu wa mpira wa wavu yamepangwa kutimua vumbi wikiendi ya Disemba 7-8 katika uwanja wa Amahoro. Timu ya Chuo Kikuu cha Utalii, Teknolojia na Biashara(UTB) ambao pia ni waandaaji wa mashindano, walishinda michuano ya kwanza mwaka jana baada ya kuikaba koo Mamlaka ya Mapato ya Rwanda(RRA) katika fainali. Timu hiyo iliendelea na kampeni zake na kushinda taji la ligi kwenye jaribio lao la kwanza na kumaliza tambo za miaka 7 za RRA baada ya kuwa mabingwa tokea mwaka 2013. Kocha mkuu wa UTB Silvestre Mbanza amesema lengo lao ni kushinda taji kwenye msimu ujao wa 2019/2020 na kwamba toka mwezi uliopita wameanza kufanya mazoezi makali kuhakikisha linatokea hilo. Msimu mpya wa ligi ya voliboli ya wanawake utaanza mwishoni mwa mwezi ujao, hata hivyo tarehe rasmi bado haijatangazwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako