• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakosoa kauli isiyowajibika kuhusu mzozo kati ya Palestina na Israel

    (GMT+08:00) 2019-11-21 09:29:10

    Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ametoa wito wa kuacha kauli na vitendo visivyowajibika vinaweza kuchochea mgogoro kati ya Palestina na Israel.

    Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu mgogoro huo, balozi Zhang amesisistiza umuhimu wa kusimamisha kauli na vitendo vinavyokwenda kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa na makubaliano ya kimataifa, na kushikilia lengo kuu la ufumbuzi wa kuwepo kwa nchi mbili. Amesema ufumbuzi wa nchi mbili na kanuni ya ardhi kwa ajili ya amani ni mstari wa mwisho wa haki ya kimataifa, na haitakiwi kuachwa hata kwa hatua moja nyuma, na kuanzisha nchi huru ni haki ya lazima ya kitaifa kwa watu wa Palestina.

    Amesema azimio nambari 2334 la Baraza la Usalama limedhihirisha kuwa ujenzi wa makazi ya wayahudi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa ikiwemo Jerusalem Mashariki zinakiuka sheria ya kimataifa.

    Habari nyingine zinasema waziri mkuu wa Palestina Mohammad Ishtaye ameihimiza jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua dhidi ya waisrael wanaoishi katika makazi Ukingo wa Magharibi wakiwa na uraia wa nchi mbili, ambao wanapatiwa ruzuku kutoka kwa serikali ya Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako