• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Aussems awekwa kando rasmi Simba

    (GMT+08:00) 2019-11-21 18:24:48

    Uongozi wa klabu ya Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wamemweka kando kocha mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems katika mechi ya ligi dhidi ya Ruvu Shooting itakayochezwa jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Simba imefikia uamuzi huo kutokana na kukerwa na tabia ya kocha huyo kuondoka nchini na kudaiwa kwenda kwao Ubelgiji kwa matatizo binafsi bila ruhusa ya mwajiri wake, hata hivyo, inadaiwa kuwa hakwenda Ubelgiji bali alikuwa nchini Afrika Kusini. Inasemekana kuwa alikwenda nchini humo kufanya mazungumzo ya kujiunga na klabu ya Polokwane inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako