• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Aliyekuwa bingwa wa Barcelona Samuel Eto'o, ajiunga na Chuo Kikuu cha Harvard

    (GMT+08:00) 2019-11-21 18:30:38

    Mwanasoka nguli mstaafu kutoka nchini Cameroon Samuel Eto'o, ameamua kurejea chuoni kupata masomo. Eto'o anaripotiwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Harvard kusomea usimamizi wa biashara ili kupata ustadi wa kudhibiti biashara yake. Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon Indomitable Lions, alisema atarejea masomoni mwezi Januari 2020. Eto'o ametambua kuwa soka inahitaji mazoezi ya kimwili na nguvu lakini kuongoza kampuni kunahitaji nguvu ya akili na maadili. Hakuna anayefahamu hatma ya biashara ya Eto'o miaka michache ijayo baada ya kufuzu katika masomo katika chuo cha Harvard.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako