• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soko la hisa la Uganda lafufuka, shughuli zaongezeka

  (GMT+08:00) 2019-11-21 19:42:55

  Mauzo katika soko la hisa la Uganda (USE) yameimarika na kufikia Shs58.2b katika kipindi cha kati ya Januari na Novemba.

  Kuimarika huko ni ishara kwamba shughuli zimeboreka katika soko la hisa tofauti na kipindi sawa na hicho mwaka jana.

  Mauzo yanafafanuliwa kama viwango vya hisa vilivyouzwa katika soko la mtaji katika muda maalum.

  Akizungumza jana jijini Kampala,Afisa Mkuu Mtendaji wa USE,Bw Paul Bwiso,alisema shughuli za soko ni bora kuliko mwka jana wakati ambapo soko hilo liliandikisha utendaji mbovu.

  USE kipindi sawa na hicho mwaka jana,liliandikisha Shs45b tu tofauti na Shs287b ambazo soko hilo liliandikisha mwaka 2016 na Shs100b mwaka 2017.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako