• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa taifa wa China kufanya ziara nchini Japani

    (GMT+08:00) 2019-11-21 20:29:34

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje Bw. Wang Yi ataongoza ujumbe kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la nchi 20 (G20) na kufanya ziara rasmi nchini Japani.

    Bw. Geng amesema, hivi sasa hatua za upande mmoja na kujilinda kibiashara vimeharibu vibaya utaratibu wa kimataifa, na uchumi wa dunia unakabiliana na hatari na hali isiyo na uhakika. Katika mkutano huo, Bw. Wang atashiriki kwenye majadiliano kuhusu kuhimiza biashara huria na usimamizi wa mambo ya dunia, maendeleo endelevu na mambo ya Afrika, na kueleza kwa kina mapendekezo na maoni kuhusu hali ya uchumi wa dunia, biashara, fedha na maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako