• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • VOLLEYBALL: Presha kwa KCB inapotafuta umalkia wa voliboli

  (GMT+08:00) 2019-11-22 18:04:51

  Baada ya kutumia fedha nyingi kuimarisha kikosi chake mwezi Desemba mwaka jana, klabu ya KCB ina presha inapofukuzia taji lake la kwanza kabisa la Ligi Kuu ya Voliboli ya wanawake itakayoingia mkondo wa lala-salama katika ukumbi wa kimataifa wa Kasarani kuanzia leo. Wanabenki hao, ambao leo hii wamekutana na timu ya DCI katika mechi ya kwanza, walinyakua kocha wa timu ya taifa Japheth Munala pamoja na wachezaji nyota akiwemo Leonida Kasaya, Noel Murambi na Violet Makuto, na Christine Njambi, na mshambuliaji matata wa Rwanda Ernestine Akimanizanye. Vipusa wa Munala wataingia awamu hii inayohusisha timu zilizokamilisha msimu wa kawaida katika nafasi nne za kwanza, na presha kali ya kuonyesha kuwa iliwekeza vyema.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako