• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Museveni aunga mkono mihuri ya ushuru ya dijitali

  (GMT+08:00) 2019-11-22 18:26:48
  Rais Yoweri Museveni ameunga mkono utekelezaji wa mihuri ya ushuru ya dijitali kwa bidhaa zinazotengenezwa nchini Uganda.

  Akizungumza kwenye Mkutano wa Ushuru wa Afrika, Museveni aliwaambia watoza ushuru kutoka Afrika, kwamba hatua mpya ya kufuatilia uzalishaji wa kampuni za utengenezaji itasaidia kupunguza udaganyifu.

  Hatua hiyo mpya ya kuanza kutumia mihuri ya ushuru ya dijiti ilizinduliwa na Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA), mnamo Novemba 1 na inawataka watengenezaji wa soda, bia, maji ya chupa na sigara kuweka stempu za ushuru za dijitali kwenye bidhaa zao.

  Hata hivyo watengenezaji watakuwa na kipindi cha neema cha miezi mitatu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako