• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Matatizo ya wakulima Arusha kukabiliwa

  (GMT+08:00) 2019-11-22 18:28:11
  Zaidi ya taasisi 12 za utafiti wa kilimo mkoani Arusha, zimeungana kwa ajili ya kutafuta njia mbadala za kutatua matatizo yanayowakabili wakulima wa vijijini Wilaya ya Arumeru.

  Akizungumza na watatifi hao, Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru, James Mchembe, alisema, hatua ya kuwakutanisha watafiti hao, itasaidia kutatua matatizo yanayowakabili wakulima katika sekta ya kilimo wilayani humo.

  Mchembe alisema, kitendo cha kuwakutanisha watafiti hao, kinalenga kuanzishwa kwa jopo la wataalamu wa kilimo ambao watapita vijijini kusikiliza kero za wakulima.

  Naye kaimu Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii ya Tengeru, Dk. Bakari George, alisema Wilaya ya Arumeru ina taasisi nyingi za utafiti hivyo, ni wajibu wao kuungana na kuwa kitu kimoja kutatua matatizo ya ardhi yanayowakabili wananchi wilayani humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako