• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mkurugenzi mkuu wa IMF

    (GMT+08:00) 2019-11-22 18:29:06

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na mkurugenzi mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Bibi Kristalina Georgieva.

    Kwenye mazungumzo yao, rais Xi amesema ukuaji wa uchumi wa dunia unapungua kwa sasa, na hatua za kujilinda kibiashara zimejitokeza, na kuuletea utaratibu wa dunia ya ncha nyingi na biashara huria changomoto kubwa, hivyo jumuiya ya kimataifa ina matarajio makubwa na utendaji kazi wa IMF.

    Ameongeza kuwa China inatetea msimamo wa utatuzi wa migogoro duniani kwa njia ya kujadili, kujenga na kunufaika kwa pamoja, na inapinga kithabiti sera ya kujilinda kibiashara, na kulinda mfumo wa biashara ya pande nyingi ambao kiini chake ni Shirika la Biashara Duniani (WTO). Rais Xi amesema China itashikilia wazo jipya kuhusu kazi za kujiendeleza, kuhimiza maendeleo yenye ubora, na kupanua ufunguaji mlango wenye ubora zaidi.

    Naye Bibi Georgieva amesema, Shirika lake litatilia mkazo na kuendelea kuimarisha ushirikiano na China, na kwamba litaunga mkono kithabiti biashara huria yenye ufunguaji mlango, kuhimiza kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja na China, na kuimarisha ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" pamoja na China.

    Wakati huohuo, rais Xi amekutana na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Henry Kissinger mjini Beijing, na kumpongeza kwa juhudi zake katika kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika miaka hiyo mingi. Amesema pande zote mbili zinapaswa kuimarisha mazungumzo juu ya masuala ya kimkakati, ili zisielewane vibaya na kuzidisha maelewano zaidi.

    Bw. Kissinger amesema nchi hizo mbili zinatakiwa kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, na kujitahidi kutafuta ufumbuzi wa kutatua mikwaruzano, na kuendelea kufanya mawasiliano na ushirikiano kwenye sekta mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako