• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Makamu wa rais wa China akutana na ujumbe wa chama tawala cha Syria

  (GMT+08:00) 2019-11-22 19:36:48
  Makamu wa rais wa China Wang Qishan amekutana na ujumbe wa chama tawala cha Syria unaoongozwa na naibu katibu mkuu wa chama hicho, Helal Helal.

  Wang amesema, China inaiunga mkono kithabiti Syria katika kulinda utawala wake, uhuru, na utimilifu wa ardhi yake, pia inawaunga mkono watu wa Syria kuamua hatma yao ya baadaye wenyewe, na kuunga mkono suluhisho la kisiasa kwa mgogoro unaoendelea nchini humo.

  Kwa upande wake, Hela amesema Syria inathamini sana urafiki na uungaji mkono wa China, na inatumai kuwa China itashiriki kikamilifu katika ukarabati mpya wa Syria baada ya vita. Amesema chama tawala cha Syria kiko tayari kushirikiana na Chama cha Kikomunisti cha China kuboresha maendeleo na mchakato wa uhusiano kati ya vyama hivyo viwili na nchi hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako