• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu wa Uingereza amesema atakamilisha mswada wa kujitoa Umoja wa Ulaya kabla ya Krismas

    (GMT+08:00) 2019-11-25 08:40:05

    Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amezindua kampeni ya uchaguzi ya chama cha wahafidhina na kuahidi kuwasilisha bungeni mswada wa kukamilisha mswada wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya Brexit kabla ya mapumziko ya Krismas ya wabunge.

    Bw. Johnson amesema mswada uko tayari, unaungwa mkono na Umoja wa Ulaya na pia unaungwa mkono na kila mwanasiasa wa chama cha Kihafidhina kwenye uchaguzi, na utasaidia kuleta wimbi la uwekezaji nchini Uingereza.

    Mbali na ahadi kuhusu kujitoa Umoja wa Ulaya, ilani ya uchaguzi aliyoitangaza pia inasema kutakuwa na kusimamisha ongezeko la kodi ya mapato, kodi ya ongezeko la thamani na michango ya bima ya taifa. Bw. Johnson ameitaja ilani hiyo kama ya kati ikilinganishwa na chama kikubwa cha upinzani cha Labour kinachoahidi matumizi makubwa ya serikali, inaahidi ajira kwa wauguzi elfu 50 na polisi elfu 20.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako