• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Syria latwaa mji kutoka kwa waasi wenye uhusiano na kundi la Al Qaeda

    (GMT+08:00) 2019-11-25 08:40:27

    Jeshi la Syria limeutwaa mji wa Misherfah ulioko kwenye jimbo la Idlib kutoka kwa wapiganaji wenye uhusiano na kundi la Al-Qaeda. Kukamatwa kwa mji huo kumetokea baada ya mapigano makali na makundi na jeshi kuharibu zana za kijeshi za waasi.

    Jeshi la Syria liliingia kwenye mji huo likiwa na ulinzi kutoka angani katika mji huo uliokuwa chini ya udhibiti wa kundi la Ajnad al-Kavkaz kundi la mrengo wa kulia linaloongozwa na Mchechnya, na washiriki wao kundi la Nusra Front.

    Jimbo la Idlib linaloonekana kama ngome ya mwisho ya waasi nchini Syria, limekuwa kimbilio la makundi ya waasi, ambako wameacha maeneo yao baada ya kusalimu amri kwa jeshi la Syria. Baadhi ya sehemu za Idlib zinahusishwa kwenye ukanda salama ulioamuliwa na Russia na Uturuki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako