• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China na Japan wapongeza kufanyika kwa mkutano wa utaratibu wa majadiliano ya ngazi ya juu kati ya nchi hizo

    (GMT+08:00) 2019-11-25 16:59:35

    Rais Xi Jinping wa China na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe wametuma barua za pongeza kwa mkutano wa kwanza wa utaratibu wa majadiliano ya ngazi ya juu kati ya China na Japan kuhusu mawasiliano baina ya watu na watu na kiutamaduni uliofanyika mjini Tokyo.

    Kwenye barua yake, rais Xi amesema dunia imeshuhudia mabadiliko makubwa ambayo hayajatokea katika miaka 100 iliyopita, na binadamu hawawezi kushughulikia changamoto za pamoja na kutafuta mustakbali mzuri bila ya nguvu ya utamaduni. Ameongeza kuwa watu wa nchi zote wanapaswa kushika na kufuata mwelekeo mkuu na kuimarisha mawasiliano ili kufungua kwa pamoja ukurasa mpya wa ustaarabu wa kibinadamu. Amesisitiza kuwa hivi sasa uhusiano kati ya China na Japan umeendelea kuboreshwa na ana matumaini kuwa nchi hizo zitatumia vizuri utaratibu huo wa kuhimiza mawasiliano kati ya watu na watu na kitamaduni, na kuongeza maelewano kati ya watu wao.

    Kwa upande wake, Bw. Abe ameeleza matumaini yake kuwa utaratibu wa majadiliano ya ngazi ya juu utaweza kuimarisha msingi wa maoni ya pamoja kwa ajili ya kujenga uhusiano kati ya Japan na China unaoendana na mahitaji ya zama mpya, na kuchangia maendeleo mapya ya uhusiano huo

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako