• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tari yapata Baraza la wafanyakazi

  (GMT+08:00) 2019-11-25 18:46:41

  Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini Tanzania (Tari) Kituo cha Uyole jijini Mbeya, imezindua Baraza la Wafanyakazi ambalo litatumika kama chombo cha kuwashirikisha wafanyakazi wote kufanya uamuzi pamoja na kuwasilisha mawazo yao kwenye ngazi za juu kwa mujibu wa sheria.

  Baraza hilo limeanzishwa kwa mara ya kwanza tangu taasisi hiyo ilipoanzishwa bila kuwapo chombo rasmi cha kuwashirikisha wafanyakazi kufanya uamuzi wa taasisi hiyo na kuwasilisha mawazo yao ngazi za juu za Serikali.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Dk. Tulole Bucheyeki, amesema kabla ya kuundwa kwa chombo hicho vilikuwa vinafanyika vikao vya utawala ambavyo ndivyo vilikuwa vinafanya uamuzi.

  Alisema vikao hivyo ndivyo vilikuwa vinafanya kazi, lakini mawazo ya wafanyakazi hayakuwa yakiwasilishwa ipasavyo kwa mujibu wa sheria za nchi, na kwamba anaamini kuundwa kwa baraza hilo kutasaidia kuboresha utendaji kazi wa taasisi.

  Katibu wa Chama cha Wafanyakazi Wanataaluma na Watafiti (Raawu), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Thomas Kasombwe, alisema kazi kubwa ya baraza la wafanyakazi ni kuwashirikisha wafanyakazi kuhusu mambo yanayofanywa na taasisi yao.

  Vile vile, alisema baraza linatakiwa kufanya kazi ya kupitisha mambo yao kwenda makao makuu ya ili yapatiwe ufumbuzi na utendaji wa taasisi uwe bora zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako