• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanawake CECAFA wataka Klabu Bingwa Wanawake

    (GMT+08:00) 2019-11-26 18:33:59

    Baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Chalenji hapo jana, viongozi wanawake kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati wameomba kuanzishwa kwa michuano ya ngazi za klabu kama ilivyo kwa wanaume ambayo ni maarufu kama Kombe la Kagame. Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) ambaye pia ni mkuu wa msafara wa timu ya nchi hiyo Bi. Doris Petra amesema, wanaamini michuano hiyo itaendelea kuwapa nafasi ya kuaimarisha zaidi wachezaji wanawake. Pia amesema hatua hiyo itakuwa ni program nyingine ya kuwajenga wachezaji wanawake ambao kwa sasa wameanza kuonyesha ushindani ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako