• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya mbioni kufufua sekta ya pamba

  (GMT+08:00) 2019-11-26 19:56:44

  Kampuni kadhaa nchini Kenya zziko mbioni kufufua sekta ya pamba nchini humo.

  Hii ni baada ya ujumebe kutoka kampuni za nguo za Thika Cloth Mills,SunFlag Textiles pamoja Knitwear manufacturing Ltd kuzuru eneo la Nyanza,ambalo ni maarufu kwa ukuzaji wa pamba,kwa lengo la kutafuta kununua pamba kutoka kwa wakulima.

  Mkurugenzi wa Thika Cloth Mills Bi Tejal Dhodhia alithibitisha kuwa serikali imejitolea kuona ya kwamba wakulima wanapewa mbegu za pamba na dawa za kupuliza kwa zao hilo la pamba.

  Meneja mkuu wa kampuni ya SunFlag Textile na Knitwear Manufacturing Ltd, Bw Vassan Shah, alisema kampuni hiyo inanunua pamba kwa wingi kutoka Uganda lakini watalenga kuzuru maeneo tofauti kukutana na wakulima wa pamba nchini Kenya ili wanunue bidhaa hiyo kutoka kwao.

  Aidha wakazi wa Siaya wamejitolea kustawisha pamba kwa wingi ili nao waweze kujiinua kiuchumi kwa kuuzia viwanda hivyo zao hilo muhimu.

  Mkurugenzi wa Thika Cloth Mills Bi.Tejal Dodhia alisema iwapo pamba itavunwa kwa wingi, bila shaka kampuni za kushona nguo zitarejelea sifa zao za hapo awali za kushona majora na kuinua uchumi wa nchi kwa kiwango kikubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako