• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali yatarajia kuunganisha watu 300,000 chini ya sera ya uunganishaji umeme bure kufikia mwisho wa mwaka

  (GMT+08:00) 2019-11-26 19:57:56

  Seriklai ya Uganda inakaribia kuunganisha watu 200,000 chini ya sera ya uunganishaji umeme bure,lakini ina pengo la uunganishaji mpya 100,000 ili kufikia malengo ya mwaka ya kuunganisha watu 300,000.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Pawakapo" iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Umeme (ERA) nchini humo,fisa Mkuu Mtendaji,Bi Ziria Tibalwa Waako,alisema takriban watu 200,00 wameunganishwa na umeme wa bure.

  Alisema wanatarajia kuunganisha watu 300,000 au zaidi kufikia mwisho wa mwaka.

  Serikali ya Uganda ilianzisha utekelezaji huu wa sera ya uunganishaji umeme bure mwezi Agosti mwaka 2018 ikiwa na mpango wa kuongeza uunganishwaji kutoka wastani wa 80,000 hadi 300,000 kila mwaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako