• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Tottenham Hotspur yaikaribisha vyema Olympiakos kwa kuibanjua 4-2

    (GMT+08:00) 2019-11-27 10:01:21

    Jose Mourinho amekuwa na mwanzo mzuri katika mechi iliyochezwa nyumbani uwanja wa Tottenham Hotspur ambapo Tottenham iliyokuwa nyuma kwa magoli mawili ilichomoka na kuizamisha Olympiakos na kuifanya kufuzu hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa. Spurs walianza kuingiwa na hofu katika nusu ya kwanza, baada ya mahasimu wao kuwachachafya kwa kuandika goli katika dakika ya sita lililoingizwa kimiani na Youssef El-Arabi na baada ya dakika 13 likapachikwa la pili na Ruben Semedo kupitia kona. Hata hivyo vijana wa Mourinho wakaamua kutulia na kuwakaribisha wageni wao vizuri kwa kuanza kuwatandika bao la kwanza dakika ya 45 kupitia Dele Alli. Kipindi cha pili Harry Kane alisawazisha dakika ya 50 na kunogewa na mpira na baadaye kuongeza lingine katika ya 77. Hata hivyo awali Serge Aurier alipachika bao la tatu dakika ya 73, na kufanya hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa Tottenham kuondoka kifua mbele kwa mabao 4-2 dhidi ya Olympiakos.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako