• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Mwanariadha kijana wa Kenya Angela Ndungwa Munguti afungiwa kwa miaka minne

    (GMT+08:00) 2019-11-28 10:25:11

    Mkimbiaji Angela Ndungwa Munguti amekuwa Mkenya wa 43 kusimamishwa mwaka huu kwa matumizi ya dawa za kusisimua misuli baada ya kufungiwa kwa miaka minne. Kwenye taarifa yake ya jana Kitengo Cha Maadili ya Wanariadha (AIU) kimesema Munguti, mwenye miaka 17 ambaye ni mkimbiaji wa zamani wa mita 800 aliyeshinda medali ya fedha kwenye michuano ya African Youth Games amegundulika kutumia Norandrosterone. Dawa hiyo ilionesha kwenye sampuli yake iliyochukuliwa Oktoba 7, 2018, kwenye program ya kudhibiti matumizi ya dawa hizo kwenye Olimpiki ya vijana wadogo ya majira ya joto iliyofanyika Buenos Aires. Marufuku yake inaanzia tarehe aliyochukuliwa vipimo. Munguti anaungana na orodha ndefu ya wakimbiaji wengine waliogundulika kutumia dawa mbalimbali za kusisimua misuli. Wanariadha 43 akiwemo bingwa wa marathon ya olimpiki 2016 Jemima Sumgong na mshindi mara tatu wa dunia wa mbio za mita 1,500 Asbel Kiprop, wamefungiwa mwaka huu. Mapema mwezi Novemba wanaridha wawili wa juu wa mbio za masafa marefu Abraham Kiptum na Cyrus Rutto, walisimamishwa kwa miaka minne na AIU.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako