• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mashabiki wa Sweden wapokea vibaya uamuzi wa Zlatan kununua klabu Sweden

    (GMT+08:00) 2019-11-29 10:39:41

    Mshambuliaji wa zamani wa timu za FC Barcelona, Inter Milan na LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic amekuwa gumzo mitandaoni kufuatia jinsi ulivyopokelewa uamuzi wake wa kununua asilimia 50 ya hisa za timu ya Hammarby inayoshiriki Ligi Kuu Sweden. Kufuatia maamuzi hayo wakati huu Zlatan akiwa kamaliza mkataba wake na klabu ya LA Galaxy ya Marekani, mashabiki wa timu yake iliyomuibua utotoni nchini kwao Sweden klabu ya Malmo wameamua kuchoma moto sanamu yake iliyokuwa imejengwa nje ya uwanja wa Malmo kwa heshima na kumuenzi mchezaji huyo. Mashabiki hao wanamuona Zlatan ni kama msaliti kwa kwenda kununua klabu pinzani, hata hivyo timu ya Hammarby na LA Galaxy zote zilikuwa chini ya umiliki wa kampuni ya AEG Sweden kabla ya Zlatan kununua hisa Hammarby.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako