• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: TP Mazembe kujenga uwanja utakaochukua mashabiki 50,000

  (GMT+08:00) 2019-11-29 18:14:07

  Mabingwa mara tano wa Afrika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, wamepanga kujenga uwanja utakaochukua mashabiki 50,000 walioketi, katika ujenzi utakaoanza mwaka ujao. Rais wa klabu hiyo yenye maskani yake makuu mjini Lubumbashi Moise Katumbi, ametangaza mpango huo jana katika hafla maalum ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo. Miongoni mwa wageni waalikwa katika hafla hiyo iliyofanyika mjini Lubumbashi, alikuwepo Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino na Rais wa CAF Ahmad Ahmad. Infantino amekiri kuvutiwa na mipango ya klabu hiyo ya DRC, na amesisitiza suala la kiongozi huyo kuendelea kupewa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha maendeleo ya soka nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako