• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Watford yamtimua kazini kocha wake Sanchez Flores

  (GMT+08:00) 2019-12-02 08:26:51

  Kocha wa klabu ya Watford Quique Sanchez Flores ametimuliwa kazini siku 85 tu baada ya kutua ugani Vicarage Road. Mhispania huyo alichukuwa wadhifa wa Javia Garcia baada ya Hornets kushiriki mechi nne za ligi bila kuandikisha ushindi wowote. Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 54 alifaulu kupata ushindi mmoja pekee katika mechi kumi za Ligi Kuu kikiwemo kichapo cha 2-1 kutoka kwa Southampton uwanjani St. Mary's. Watford wanasalia kushikilia mkia kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi nane walizopata katika mechi 14 tangu kuanza kwa msimu mpya wa 2019-20. Kulingana na ripoti ya Sky Sports, kocha wa zamani wa Brighton Chris Hughton, amehusishwa na kuwa kocha wa tatu wa Watford msimu huu mpya. Kwa sasa anakuwa kocha wa tatu kupoteza wadhifa wake katika klabu kuu ya Uingereza baada ya Mauricio Pochettino na Unai Emery.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako