• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • LANGALANGA: Lewis Hamilton aendeleza makamuzi kwenye mbio za Abu Dhabi Grand Prix

  (GMT+08:00) 2019-12-02 08:30:16

  Lewis Hamilton jana alitawala mbio za Abu Dhabi Grand Prix na kumaliza msimu akiwa ameshinda taji la sita la dunia. Dereva huyo wa Mercedes alianza kuongoza tangu mwanzo wa mbio hizo na kuendesha akiwa mbali bila ya kuwa na gari nyuma yake la kumsumbua. Katika mbio hizo Max Verstappen wa Red Bull amechukua nafasi ya pili baada ya Ferrari kuponyoka na kuwa nyuma yao. Charles Leclerc alikuwa wa pili katika mizunguko ya kwanza mbele ya Verstappen, lakini baadaye akaachwa nyuma na kuwa watatu. Leclerc alikuwa hatarini kupoteza nafasi ya tatu kwasababu kabla ya mbio FIA iligundua kuwa kiwango cha mafuta walichosema Ferrari kipo kwenye gari yake kilikuwa tofauti na kile wakati gari inaangaliwa. Lakini baada ya uchunguzi uliofanywa mbio zilipomalizika Ferrari wakarambwa faini ya €50,000. Ushindi wa Hamilton ni wa 11 katika mbio 21 zilizofanyika msimu huu, ushindi ambao ni sawa na wa mwaka 2014 na 2018.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako