• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mfumko wa bei waongezeka krimasi ikikaribia

  (GMT+08:00) 2019-12-03 19:43:48
  Kiwango cha mfumuko wa bei wa kila mwaka nchini Uganda kimeongezeka hadi asilimia 3.0 katika mwaka unaomalizika Novemba 2019 ikilinganishwa na asilimia 2.5 iliyosajiliwa katika mwaka uliopita.

  Hata hivyo mfumko huo bado ni asilimia 2.3 chini ya lengo la sera la asilimia 5.

  Ofisi ya Takwimu ya Uganda imesema kwamba kuongezeka kwa mfumuko wa bei kunasababishwa na mfumuko wa bei wa msingi wa kila mwaka, ambao uliongezeka hadi asilimia 2.9. kutoka asilimia 2.6 iliyosajiliwa mwaka uliopita kufuatia kupanda kwa bei ya nguo na viatu wakati huu wa kuelekea sikukuu ya Krisimazi.

  Akiwasilisha ripoti ya Bei ya Watumiaji ya Novemba katika Idara ya taakwimu, mkurugenzi wa Takwimu za uchumi Bi Aliziki Kaudaha Lubega alisema mfumuko wa bei wa Uganda unafuata msingi wa misimu ambao tayari serikali imetafiti.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako