• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SAFARIRALLY: Mbio za Afrika Mashariki Safari Classic Rally 2019 zatawaliwa na wageni

    (GMT+08:00) 2019-12-04 08:46:41

    Mpambano wa kuwania uongozi kwenye mbio za Afrika Mashariki Safari Classic Rally 2019 sasa unaonekana kuwepo kati ya madereva wa kigeni baada ya dereva mwenyeji aliyekuwa kwenye nafasi nzuri kuachwa nyuma kwenye mbio hizo. Jumapili Tejvir Rai alipoteza nafasi yake ya tatu huko Arusha Tanzania baada ya gari lake la Porsche 911 kuwa na hitilafu kwenye gurudumu la kulia. Kris Rosenberger kutoka Austria, anayeendesha Porsche 911 akiongozwa na Mjerumani Nicola Bleicher, jana ambayo ni siku ya sita ya mashindano aliimarisha uongozi wake. Naye Msweden Stiq Blomqvist, anayeongozwa na Jorgen Fornander ambaye pia anatoka Sweden, yupo nafasi ya pili akiendesha Porsche 911 huku Philip Kadoorie kutoka Hong Kong, China anayeongozwa na Muingereza Ryan Champion, anashika nafasi ya tatu. Dereva aliyekuwa nafasi ya juu hadi jana ni Mkenya Aslam Khan ambaye alimaliza nafasi ya tano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako