• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uzito wa mizigo iliyosafirishwa kwa reli ya SGR Kenya waongezeka kwa asilimia 12 katika miezi tisa ya kwanza

    (GMT+08:00) 2019-12-06 09:31:45

    Takwimu zilizotolewa jana na Ofisi ya takwimu ya taifa la Kenya (KNBS) zimeonesha kuwa uzito wa mizigo iliyosafirishwa kwa reli ya SGR nchini humo umeongezeka kwa asilimia 12 katika miezi tisa ya kwanza mwaka huu.

    Takwimu zinaonesha kuwa, kwenye miezi hiyo tisa treni za reli ya SGR zilisafirisha mizigo yenye uzito wa tani milioni 3.26 kutoka bandari ya Mombasa hadi Nairobi, ikilinganishwa na tani milioni 2.92 za mwaka jana wakati kama huo.

    Habari nyingine zimesema, kampuni ya reli ya Kenya imetangaza kuongeza mabehewa matano kwenye treni ya abiria ya reli ya SGR kati ya Nairobi na Mombasa, ili kukidhi mahitaji ya ongezeko la abiria.

    Mabehewa hayo ya ziada yatakayohudumia abiria wa daraja la tatu na daraja la kwanza yataongezwa kuanzia tarehe 22 mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako